Kukorogeka kwa ada baada ya vidonge

Swali: Kuna mwanamke ambaye ada yake ya mwezi ilikuwa inamjia kwa kipindi cha siku nne. Baada ya kutumia vidonge vya kuzuia mimba ada ya mwezi ikawa inamjia siku kumi ambapo siku tano za mwanzo inakuwa ni matone  madogo yalioambatana na maumivu. Ni ipi hukumu ya swalah katika zile siku tano za mwanzo?

Jibu: Huyu amejiharibia ada yake ya mwezi mwenyewe kwa kutumia tembe za kuzuia mimba. Ni kwa nini anazitumia? Muda wa kuwa damu yake ni yenye kuendelea na haikukatika inazingatiwa kuwa ni hedhi hata kama kwa sasa itaenda mpaka siku kumi na tano.  Yeye mwenyewe ndiye ambaye ameiharibu hedhi yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (28)
  • Imechapishwa: 05/02/2022