Kukojoa kwa kusimama


Swali: Je, inafaa kwa mtu kukojoa kwa kusimama pamoja na kuzingatia kwamba hakuna mkojo wowote unaofika mwilini au nguoni?

Jibu: Hapana neno kukojoa kwa kusimama khaswakhaswa pindi mtu anahitajia kufanya hivo muda wa kuwa mahali hapo pana stara na hakuna yeyote anayeona uchi wa mkojoaji na hafikiwi na chochote katika zile cheche za mkojo. Hayo ni kutokana na yale yaliyothibiti kwa Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alienda mahali ambapo watu wanatupa takatalaka ambapo akakojoa kwa kusimama. al-Bukhaariy na Muslim wameafikiana juu ya usahihi wake. Lakini bora ni kukojoa kwa kuketi chini. Kwa sababu hivo ndivo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivofanya mara nyingi, kunasitiri zaidi uchi na kunamtia mtu mbali na kufikwa na cheche za mkojo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/445)
  • Imechapishwa: 27/02/2021