Kukodisha wanawake kuja kuimba harusini

Swali: Ni ipi hukumu ya kukodisha wanaokuja kuimba nyimbo katika sherehe za wanawake za ndoa?

Jibu: Ikiwa nyimbo zake ni katika zile aina ya nyimbo zilizoruhusiwa basi hakuna neno kukodisha mwanamke aje kuimba. Lakini kwa sharti malipo yake yawe ni yenye kuingia akilini ambayo yanaendana na kazi yake. Si kama wafanyavyo baadhi ya watu ambapo katika usiku wanampa pesa 3.000 au 4.000. Mambo gani haya?

Ama ikiwa ni katika zile aina ya nyimbo za haramu kama zile nyimbo za wanawake wachafu na makahaba ni haramu. Ni mamoja mkampa malipo au msimpe malipo. Tofauti ni kwamba nyimbi zilizoruhusiwa ni kazi iliyoruhusiwa. Kile ambacho kimeruhusiwa inaruhusiwa vilevile kuchukua malipo kwa ajili yake. Kuhusu nyimbo ya haramu ni haramu. Allaah akiharamisha kitu anaharamisha vilevile thamani yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (36) http://binothaimeen.net/content/799
  • Imechapishwa: 22/01/2018