Kukitolea zakaah kiwanja ambacho mtu hana lengo la kukiuza

Swali: Ni wajibu kuitolea zakaah ardhi ambayo mtu amepokea kutoka katika nchi pamoja na kuzingatia kwamba hataki kujenga makazi?

Jibu: Ni lazima kwake kuitolea zakaah. Kwa sababu mtu huyu si mwenye kufanya biashara ya viwanja. Lakini ameibakiza kwa lengo akiihitaji ataiuza na vinginevyo itabaki. Kadhalika kama ni mwenye kusita kati ya kuifanyisha biashara au kuibakiza kwa lengo la kujenga nyumba na mfano wa hayo. Kilicho muhimu ni kwamba mtu huyu halazimiki kutoa zakaah. Vivyo hivyo iwapo mtu atanunua ardhi kwa sababu ya kuifanyisha biashara na katikati ya mwaka akaanza kujenga nyumba [kwa ajili ya kukaa ndani yake], basi aradhi hiyo haina zakaah.  Kadhalika iwapo atanunua ardhi ili ajenge kisha nafsi yake ikampendeza na akaitangaza kwa ajili ya kuiuza kwa lengo anunue ardhi nyingine, ardhi hii haina zakaah. Zakaah ya viwanja ni lazima kwa wale wanaofanya biashara ya viwanja. Nao ni wale wafanya biashara ya majengo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (71) http://binothaimeen.net/content/1630
  • Imechapishwa: 26/03/2020