Kukimu muadhini ambaye hakutoa adhaana

Swali: Kuna muadhini anaadhini wakati mwenzake hayupo ambapo anakuja mtu mwengine na kukimu swalah na anamkataza yule muadhini wa kwanza kukimu. Je, huyu ana haki ya kufanya hivo?

Jibu: Msingi ni kwamba muadhini ndio mwenye kukimu. Endapo atakimu mwengine hakuna neno. Lakini lililo  bora ni kwamba yule muadhini ndiye anatakiwa kusimamia kukimu. Iwapo atasimamia mwengine hakuna neno.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 23/03/2018