Kukidhi swalah zilizompita mtu maishani ijumaa ya mwisho ya Ramadhaan


Swali: Nimesoma katika kitabu kilichotungwa na ´Abduh Muhammad mlango ambao una faida inayosema: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule aliyepitwa na swalah katika maisha yake na asiidhibiti, basi asimame kuswali ijumaa ya mwisho ya Ramadhaan na aswali Rak´ah nne kwa Tashahhud moja. Rak´ah ya kwanza atasoma al-Faatihah na Suurah “al-Qadr” na “al-Kawthar” mara kumi na tano. Manuizi atasema:

“Nimenuia kuswali Rak´ah nne ikiwa ni kafara juu ya zile swalah zilizonipita.”

Je, mambo haya ni sahihi?

Jibu: Mambo haya hayana msingi wowote. Ni mambo yaliyoundwa na ya uongo. Mambo haya hayana msingi wowote. Bali ni mambo ya uongo na ya batili. Mtu kama amepitwa na swalah na haikumbuki, basi ajitahidi kukumbuka ni ipi; Dhuhr, ´Aswr, Maghrib, ´Ishaa, Maghrib au ´Ishaa kisha atende kazi kwa mujibu wa dhana yake na aswali kwa mujibu wa vile dhana yake ina nguvu zaidi. Anaweza kuikidhi wakati wowote.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb https://binbaz.org.sa/fatwas/7608/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%82%D8%B6%D8%A7%D8%A1-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D9%88%D8%A7%D8%AA-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D8%AE%D8%B1-%D8%AC%D9%85%D8%B9%D8%A9-%D9%85%D9%86-%D8%B1%D9%85%D8%B6%D8%A7%D9%86-%D9%84%D9%85%D9%86-%D9%81%D8%A7%D8%AA%D8%AA%D9%87-%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9
  • Imechapishwa: 21/05/2020