Kukidhi swalah zilizompita mtu maishani ijumaa ya mwisho ya Ramadhaan II

Swali: Nimesoma kwenye kitabu maneno kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) eti amesema:

“Yule aliyepitwa na swalah katika maisha yake na asiidhibiti, basi asimame kuswali ijumaa ya mwisho ya Ramadhaan na aswali Rak´ah nne kwa Tashahhud moja. Katika kika Rak´ah atasoma al-Faatihah na Suurah “al-Qamar” na “al-Kawthar” mara kumi na tano. Manuizi atasema:

“Nimenuia kuswali Rak´ah nne ikiwa ni kafara juu ya zile swalah zilizonipita.”

Akimaliza kuswali atamswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mara mia moja.”

Je, swalah hii ni sahihi?

Jibu: Khabari hizi ni za kutungwa na amesemewa uongo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hazina ukweli wowote. Yote haya ni uongo. Yule aliyepitwa na swalah, ikiwa amepitiwa na usingizi au amesahau, basi aiswali na kuilipa. Ama ikiwa alikusudia kuacha swalah basi mtu huyu ni lazima kwake kutubu kwa Allaah. Akiilipa ni sawa na si lazima kuikidhi. Tawbah inatosha. Akitubu kwa Allaah na akajutia zile swalah zilizompita itamtosha. Kwa sababu kuacha swalah ni ukafiri mkubwa. Inatosha kwa mtu kutubia juu ya ukafiri. Allaah (Subhaanah) amesema:

قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا إِن يَنتَهُوا يُغْفَرْ لَهُم مَّا قَدْ سَلَفَ

“Waambie wale waliokufuru kwamba wakikoma watasamehewa yaliyotangulia.”[1]

Yeyote mwenye kuacha swalah kwa makusudi amekufuru. Na ikiwa anapinga kwamba ni lazima basi amekufuru kwa maafikiano. Lililo la wajibu kwake ni yeye kutubu juu ya jambo hilo. Ama ikiwa ni kwa kusahau au kupitiwa na usingizi, mtu huyu pindi atapoamka au atapokumbuka ataharakisha kuswali.

[1] 08:38

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb https://binbaz.org.sa/fatwas/10302/%D8%A7%D9%84%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B9%D9%84%D9%89-%D8%AD%D8%AF%D9%8A%D8%AB-%D9%85%D9%86-%D9%81%D8%A7%D8%AA%D8%AA%D9%87-%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D9%81%D9%8A-%D8%B9%D9%85%D8%B1%D9%87-%D9%88%D9%84%D9%85-%D9%8A%D9%82%D8%B6%D9%87%D8%A7-%D9%81%D9%84%D9%8A%D9%82%D8%B6-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D8%AE%D8%B1-%D8%AC%D9%85%D8%B9%D8%A9-%D9%85%D9%86-%D8%B1%D9%85%D8%B6%D8%A7%D9%86
  • Imechapishwa: 21/05/2020