Kukataza madhambi wakati wa kwenda sokoni


Swali: Wakati wa kwenda sokoni mtu huona madhambi mengi. Tunatakiwa kushika msimamo gani? Je, tuwakataze?

Jibu: Unajua jibu:

“Yule katika nyinyi atakayeona maovu basi ayazuie kwa mkono wake. Asipoweza kufanya hivo, afanye hivo kwa mdomo wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa moyo wake – na hiyo ni imani dhaifu kabisa.”[1]

Swali: Ikiwa mtu anaweza kukataza kwa mdomo wake. Je, awakataze wale wote wanaotenda dhambi njiani wakati wa kwenda sokoni?

Jibu: Unakanyaga maji. Jibu ni lile lile juu ya swali hili:

“Yule katika nyinyi atakayeona maovu basi ayazuie kwa mkono wake. Asipoweza kufanya hivo, afanye hivo kwa mdomo wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa moyo wake – na hiyo ni imani dhaifu kabisa.”

Je, anaweza kukataza kila dhambi anayoiona? Ima anaweza kufanya hivo au hawezi kufanya hivo. Jibu ni lile lile.[1] Ahmad (03/10) na Muslim (49).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Raabigh (02)
  • Imechapishwa: 16/09/2017