Kukataa Shari´ah miongoni mwa Shari´ah za Kiislamu

Kuna pote la wanachuoni lililosema kuwa kundi linalokataa kushikamana na Shari´ah miongoni mwa Shari´ah za Uislamu, linauawa, pasi na kujali ikiwa Shari´ah hiyo itakuwa ni wajibu au imependekezwa. Kwa mfano wakakusanyika watu na kusema “sisi tutashikamana na hukumu za Kiislamu zote lakini hatushikamani na adhaana”, bi maana wakakataa adhaana na kusema si ya kwao bali ni ya kundi katika Ummah mwingine. Mfano mwingine wakasema “sisi tutashikamana na hukumu za Kiislamu isipokuwa Zakaah tu na si wajibu kwetu kumpa nayo kiongozi”, bi maana wanaamini kuwa kuna kitu miongoni mwa mambo ya Shari´ah kisichoingia ndani ya Shari´ah. Mfano wa watu sampuli hii ni kama wale waliokataa kutoa Zakaah katika wakati wa Abu Bakr, wale waliodai kuwa mambo ya ´ibaadah sio wajibu kwao au swalah na Zakaah, zinaa sio haramu kwao na mfano wa hayo.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 173-174
  • Imechapishwa: 17/05/2020