Kukariri al-Faatihah katika Rak´ah moja


Swali: Imamu akirefusha kusoma al-Faatihah katika Rak´ah mbili za mwisho. Je, naweza kukariri kisomo mara ya pili?

Jibu: Hapana. Nguzo haikaririwi. Usikariri al-Faatihah katika Rak´ah moja. Usikariri. Nyamaza au unaweza kuleta Dhikr; Tasbiyh, Tahliyl n.k. Hakuna neno. Au unaweza kumuomba Allaah msamaha na rehema.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ls--1428-03-01.mp3
  • Imechapishwa: 21/09/2020