Swali: Kuna mtu anasafiri wakati mwingine siku ya Ijumaa. Hivyo anaswali Ijumaa kama Dhuhr. Je, inajuzu kwake kujumuisha Swalah ya ´Aswr pamoja na ´Dhuhr siku ya Ijumaa?

Jibu: Ndio. Akiswali Dhuhr siku ya Ijumaa au siku nyingine ajumuishe pamoja na ´Aswr. Kilichokatazwa ni kujumuisha ´Aswr na Ijumaa. Hili ndio limekatazwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Sharh Zaad-il-Ma´aad (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-5-23.mp3
  • Marejeo: Firqatunnajia.com
  • Imechapishwa: 09/11/2014