Kujitutumua kwa al-Hajuuriy kwamba hakumvulia adabu Mtume صلى الله عليه وسلم


al-Hajuuriy amesema alipokuwa akijitetea:

”Hakuna ndani ya maneno haya kumtukana (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Bali ni kumsifu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Shari´ah yake tukufu. Kwa kuyatilia nguvu [niliyoyasema] ni Wahy uliyokuja kutia adabu pamoja na mtiririko wa maneno ambayo ndani yake kuna kubainisha aina za Sunnah. Yote haya yanathibitisha kumuadhimisha Mtume huyu na Shari´ah yake iliyotwaharika. Ndani yake hakuna matusi kwa wenye busara na inswafu.”

Halafu akasema:

”Pamoja na hayo pindi baadhi ya watu walipoyafasiri maneno yangu kimakosa, jambo ambalo halipelekewi na maneno yangu, na wakakataa mtiririko unaobainisha maneno haya na mfano wake, ndipo nikasema: ”Mimi najirudi kutokamana na usulubu huu na ninamuomba Allaah msamaha kwayo ili kukata mzizi wa fitina unaokusidiwa na baadhi ya watu.”

al-Hajuuriy anaendelea kung´ang´ania ya kwamba hakufanya makosa juu ya cheo cha utume na kujirudi huku ni kwa sababu tu ya kukata mzizi wa fitina unaokusudiwa na baadhi ya watu.

Ninaapa kwa Allaah ya kwamba maneno haya ya al-Hajuuriy ndio fitina yenyewe. Ninamshauri kukimbilia kutubu kwa Mola Wake ambaye ndiye muumba na bwana Wake. Ndugu! Tubu kwa maneno haya mabaya kuhusu Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Huko mbele yatakuja maneno ya Shaykh al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) ya kwamba maneno haya – maneno ya al-Hajuuriy – ni mabaya na maovu.

  • Mhusika: Shaykh ´Arafaat bin Hasan bin Ja´far al-Muhammadiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan al-Fawriy (01/09)
  • Imechapishwa: 11/10/2016