Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ambaye yatamshinda matapishi basi halazimiki kulipa. Na ambaye atajitapisha basi ni lazima kwake kulipa.”[1]

Ni ipi maana ya Hadiyth hii?

Jibu: Maana yake ni pale ambapo mfungaji atasababisha kutapika swawm yake inabatilika. Kwa sababu ametoa chakula kwenye tumbo lake na hivyo swawm yake inaharibika.

[1] Abu Daawuud (2380), at-Tirmidhiy (720), Ibn Maajah (1676) na Ahmad (10468). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaami´ (6243).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (14) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–14330720.mp3
  • Imechapishwa: 09/06/2020