Kujionyesha katika mambo ya kidunia kazini

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu akajionyesha katika mambo ya kidunia kwa mfano mwajiriwa akaonyesha bidii zaidi mbele ya bosi wake kazini?

Jibu: Haijuzu kufanya hivi. Ni katika jukumu la kazi. Ni katika dini. Haifai kuonyesha bidii na ijitihadi mbele ya bosi na akazembea wakati bosi hayuko. Haijuzu kufanya hivi. Kazi iko katika dhimma yako sawa akiwepo bosi au asiwepo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (87) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul%20Majd-3-7-1439.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2018