Swali: Ni ipi hukumu ya kujiliza kwa pamoja kwa sauti ya juu msikitini kwa ajili ya kuleta unyenyekevu?

Jibu: Kujiliza kwa feki, kama wanavyofanya baadhi ya watu, ni kitu hakikuwekwa katika Shari´ah. Kuhusu machozi yanayotoka kwa ajili ya unyenyekevu wa moyo, kuhisi ukubwa wa Mola na kwa ajili kumuogopa ni jambo limewekwa katika Shari´ah. Sauti ikisikika bila ya yeye kujifanyisha hilo wala kujikakama, ni sawa. Ama kujiliza ambako ni feki ni kitu hakikuwekwa na wala hakitakikani. Kinachotakiwa ni mtu ayazingatie maneno ya Allaah (´Azza wa Jall). Akiyazingatia kwa ukweli na hali ya kuwa anaelewa maana, bila ya shaka moyo wake utakuwa mlaini, utaogopa na kulia pale kunapotajwa adhabu anaogopa, na pale kunapotajwa thawabu anaingiwa na matumain, na pindi anapotajwa Mola kwa ajili ya kumuadhimisha, na pindi anapotajwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na historia yake kwa ajili ya kumpenda na kuwa na shauku nae.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (05)
  • Imechapishwa: 03/05/2020