Swali: Baadhi ya wanafunzi wanasema kuwa haimpasi yeyote kusema: “Mimi ni Salafiy”, kwa kuwa katika hili kuna utakaso wa nafsi.

Jibu: Ikiwa anasema hili kwa ajili ya kujitakasa nafsi yake, haijuzu. Ni kweli. Ama ikiwa anasema kwa ajili ya kubainisha, kwa kuwa yuko kati ya mapote na makundi yanayokwenda kinyume na anajitenga nao na kusema: “Mimi ni Salafiy na niko katika Manhaj ya Salaf” kwa ajili ya kujiweka mbali, hili ni jambo zuri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://youtu.be/ofcxcsHeN3E
  • Imechapishwa: 09/11/2014