Kujifunza elimu ya Shari´ah kwa ajili ya kazi

Swali: Mimi ni mwanafunzi na kutafuta kwangu elimu ni kwa ajili ya kuajiriwa au kuchuma pesa. Je, inafaa kukusanya kati ya nia ya dini na dunia?

Jibu: Kilicho cha lazima ni kuitakasa nia na kuifanya kwa ajili ya Allaah pekee ili kuijua hukumu ya Allaah na yale uliyoumbiwa kwa ajili yake. Lengo jingine ni ili uweze kuifanyia kazi Shari´ah ya Allaah kwa ujuzi na hilo jambo la pili linakuwa lenye kufuatia. Riziki inatoka kwa Allaah. Ni lazima kufanya kazi kwa ajili ya kutafuta riziki. Lakini nia ya kujifunza elimu inatakiwa iwe kwa ajili ya Allaah pekee. Kisha ukishapata elimu hapana vibaya kujiajiri au kufanya kazi za kujitegemea ambazo hazina uhusiano wowote na kazi.

Kuhusu kujifunza elimu kwa ajili ya kazi ni khasara kubwa na kosa kubwa. Lakini muumini anaweza kunuia hivo kisha akawafikishwa kuwa na nia njema. Baadhi ya Salaf wamesema:

“Tumetafuta elimu kwa ajili ya dunia… “

Imekuja katika tamko jingine:

“Tumetafuta elimu kwa ajili ya asiyekuwa Allaah lakini ikakataa kuwa isipokuwa kwa ajili ya Allaah.”

Mwanafunzi anaweza kujifunza elimu kwa ajili ya kazi au kutokana na sababu nyingine, kisha akasaidiwa na kuwafikishwa kumtakasia nia Allaah.

Kwa kuhitimisha ni kwamba mwanafunzi anatakiwa kupambana na apambane na nafsi yake ili kule kusoma kwake kuwe kwa ajili ya Allaah. Nia hii inayomtia wasiwasi na kumsumbua aipige vita kiasi na anavyoweza ili kusoma kwake kuwe kwa ajili ya Allaah pekee. Baadaye kazi na dunia vitakuja.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4275/حكم-طلب-العلم-للوظيفة-والدنيا
  • Imechapishwa: 12/06/2022