Wanafalsafa hawakupinga misingi ya dini waziwazi. Kwa kuwa lau wangelikanusha misingi ya imani watu wangelijua ukafiri wao waziwazi. Walichofanya ni kuwatia watu mchanga wa machoni kwa kuwa watu hawa ni wanafiki na mazanadiki na wamejificha nyuma ya Uislamu. Wanathibitisha misingi ya imani hii kimatamshi lakini hawafanyi hivo kihakika. Hawakumuamini Allaah, Malaika Wake, Kitabu Chake, Mtume Wake, siku ya Mwisho kihakika.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/431)
  • Imechapishwa: 19/05/2020