Kujiepusha na mambo yenye kutia shaka     

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

06- Abu ´Abdillaah an-Nu’maan bin Bashiyr (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa alimsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“…. yule anayeepuka vyenye shaka atakuwa amejisafisha kwenye dini yake na heshima yake.”

Akijiepusha atakuwa amefanya wajibu wake. Hakimbilii kufanya kitu asichojua hukumu yake kwa sababu huenda ikawa ni haramu. Muumini ambaye ´ibaadah ni wajibu kwake inatakiwa kwake kwa njia ya uwajibu asifanye kitu isipokuwa awe na utambuzi ya kuwa ni halali au haramu. Mwenye kujiepusha na halali inayotia shaka au haramu inayotia shaka atakuwa amejisafisha kwenye dini kwa kuwa huenda akafanya jambo hilo na ikawa ni haramu na yeye hajui. Mtu anaweza kusema kuwa ni mwenye kupewa udhuru kwa vile hajui?

Jibu ni: hapana, sio mwenye kupewa udhuru kwa kuwa lililokuwa la wajibu kwake ni kukomeka mpaka imbainikie hukumu ya mambo haya. Yeye ni mtu ambaye ´ibaadah ni yenye kumuwajibikia (Mukallaf). Hivyo basi, hafanyi kitendo chochote isipokuwa kwa maamrisho kutoka kwenye Shari´ah. Ndio maana amesema (´alayhis-Swalaatu was-Salaam):

“… atakuwa amejisafisha kwenye dini…”

Kisha akasema pia:

“… na heshima yake.”

Kwa kuwa mwenye kufanya mambo yenye kutia shaka miongoni mwa watu wenye imani, kuna uwezekano watu wakaanza kumsema vibaya ya kwamba hana msimamo kwa kuwa hakujisafisha na dini yake. Kwa njia hiyo akijiepusha na vyenye kutia shaka atakuwa ameisafisha heshima yake.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 148-149
  • Imechapishwa: 17/05/2020