Kujibunia hukumu katika nchi isiyohukumu kwa Shari´ah

Swali: Tunaishi katika nchi isiyohukumu kwa Shari´ah. Kunatokea uzinzi na tuhumu kati ya waislamu. Ni ipi hukumu lau tutalipa kima fulani cha pesa kwa yule aliyetuhumiwa kimakosa au kwa mume ambaye mke wake ameziniwa na wakati huo huo kuwabainishia watu uhalisia wa hukumu ya Allaah juu ya suala hilo lakini tunafanya hivo kwa sababu ndicho kinachowezekana. Je, huku ni kuhukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah?

Jibu: Ndio. Usihukumu. Msihukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah. Allaah hakuwapeni jukumu la kuhukumu kati ya watu kinyume na Qur-aan na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (41) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%204%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 13/03/2017