Kujiazima kutoka katika zakaah

Swali: Nafanya kazi ya kukusanya swadaqah na zakaah kutoka kwa watenda wema. Baadhi ya nyakati huhitaji kukunua kitu kutoka katika pesa hizi. Je, inafaa kwangu kujiazima nazo kisha baadaye nizirejeshe?

Jibu: Hapana, haijuzu kwako kufanya hivo. Hii ni amana mikononi mwako. Usichukue chochote kutoka katika amana.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (15)
  • Imechapishwa: 28/06/2020