Swali: Neno “Khawaarij” anaambiwa yule mwenye kufanya uasi kwa mtawala wa waislamu peke yake au yule ambaye amekusanya I´tiqaad zote mbovu za Khawaarij ikiwa ni pamoja na kupinga uombezi, kukufurisha kwa dhambi kubwa na kuwafanyia uasi watawala? Anaambiwa nini yule mwenye kuamini baadhi ya I´tiqaad zao tu?

Jibu: Mwenye kuitakidi baadhi ya I´tiqaad zao, yeye ni kama wao. Akiitakidi I´tiqaad zao zote, huyu ni mbaya zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (04) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2107
  • Imechapishwa: 01/07/2020