Kuitwa ´Abuud na ´Ubaydullaah badala ya ´Abdullaah

Swali: Ni ipi hukumu ya kuyafupisha majina yenye maana ya kumwabudu Allaah (´Azza wa Jall) kama mfano wa kusema ´Abuud badala ya ´Abdullaah?

Jibu: Hakuna neno kuyafupisha. Kwa sababu hawamaanishi kulifupisha jina la Allaah (´Azza wa Jall). Wanachokusudia ni kufupisha yule mwenye kuitwa. ´Abdullaah wanamwita ´Ubaydullaah. Hakuna neno katika hili. Baadhi yao wanasema ´Ubuud. Hakuna neno katika hili. Baadhi yao ´Abdur-Rahmaan wanasema ´Ubayd-ur-Rahmaan. Hakuna neno katika hili. Baadhi yao husema Tuhaym. Hili pia halina neno. Ufupikaji wanachokusudia ni kumfupiza yule mwenye kuitwa na sio kufupiza jina la Allaah tukufu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (66) http://binothaimeen.net/content/1486
  • Imechapishwa: 24/01/2020