Kuitika mwaliko wa chakula wa ndugu ambaye anakula ribaa

Swali: Kuna mtu anafanya kazi sehemu ya ribaa na hana pato lingine zaidi ya hili. Vipi tutangamane nae na chakule chake akitualika kwake ilihali ni miongoni mwa watu ambao ni wajibu kuwaunga?

Jibu: Mkijua kuwa chakula hichi kinatokamana na pato la haramu basi msile. Ama ikiwa ana pato la haramu na zuri ambalo ni halali basi kuleni midhali kile mnachokula hamjui kuwa kinatokamana na pato la haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anakula chakula cha mayahudi ilihali wanakula ribaa. Alifanya hivo wa sababu hakuwa na yakini kile anachokula kuwa kinatokamana na ribaa. Kwa kuwa wana mali zengine ambazo si ribaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/02-02.mp3
  • Imechapishwa: 20/11/2017