Kuitia Qur-aan kwenye maji


Swali: Baadhi ya wafanya matabano wanaandika Qur-aan kwenye makaratasi kisha wanayaweka makaratasi hayo ndani ya maji mpaka yale maandishi yanapotea. Halafu wanamuamrisha mgonjwa kuoga maji hayo. Je, inajuzu?

Jibu: Ndio, hakuna neno. Anaweza kuyanywa na kuyaoga. Ni katika kujitibu na aina moja wapo ya matabano. Hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (64) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/28-07-1438h-fathou.mp3
  • Imechapishwa: 29/07/2017