Kuitanguliza zakaah kabla ya wakati wake

Swali: Kuna mwanamke anamiliki dhahabu ambapo akakusanya zakaah yake mpaka ufike wakati wa kuitoa. Shangazi yake akaja kutoka mji mwingine ambaye alikuwa katika hali ya kuhitaji ambapo akachukua sehemu ya zakaah yake na kumpa shangazi yake kabla ya kufika wakati wa kuitoa. Je, ni sahihi kule kuitoa kwake?

Jibu: Inafaa kwake kuitanguliza zakaah yake kabla ya wakati wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alichukua zakaah ya miaka miwili kutoka kwa ami yake al-´Abbaas. Hivyo inafaa kuitanguliza zakaah kwa ajili ya maslahi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (10) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191426#219753
  • Imechapishwa: 06/05/2019