Swali: Unasemaje juu ya msomaji Qur-aan anayesoma kwa maqaamaat inayofanana na nyimbo?

Jibu: Haijuzu kwa muumini kusoma Qur-aan kwa mtindo wa nyimbo na waimbaji. Bali analazimika kuisoma kama walivoisoma Salaf ambao ni Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wale waliowafuata kwa wema. Aisome kwa utararibu ipasavyo, hali ya kuwa na huzuni na unyenyekevu ili iathiri mioyo ya wasikilizaji na yeye mwenyewe aathirike nayo. Kuisoma kwa mfumo wa waimbaji ni jambo lisilojuzu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (09/290)
  • Imechapishwa: 17/07/2021