Swali: Muulizaji kutoka Ufaransa anasema kuwa alioa mwanamke ilihali wote wako na watoto wadogo. Baada ya hapo nikaja kujua kuwa mke wangu anatumia madawa ya kulevya. Ni ipi nasaha yako na inajuzu kwangu kumtaliki kwa sababu hii?

Jibu: Si kwamba inajuzu, bali ni wajibu kwako kumtaliki maadamu anatumia madawa ya kulevya. Huyu ataiharibu nyumba yako na atakuharibia watoto wako. Wewe unamlimbikiza ilihali ni mujrima. Ni juu yako kufanya haraka kumtaliki na kutengana naye. Isipokuwa tu ikiwa kama atatubu tawbah sahihi na akaacha kutumia madawa ya kulevya. Katika hali hii atakuwa ni mke wako. Ama ikiwa ataendelea si sawa akabaki.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (05) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2124
  • Imechapishwa: 01/07/2020