Kuirudi al-Faatihah Kwa Kukosa Unyenyekevu

Swali: Wakati mwingine wakati ninaposoma al-Faatihah katika swalah ninairudi kwa sababu ninaonelea kuwa nimeisoma mbio mbio pasi na mazingatio…

Jibu: Hapana. Usomaji wa al-Faatihah ni nguzo na nguzo haikaririwi. Nguzo haikaririwi katika swalah. Inatosheleza kuisoma mara moja. Ni kama Sujuud; huwezi kusujudu kwa mara ya pili au tatu au ya nne. Nguzo haikaririwi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20%20-%2017-%2010-1436.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017