Kuipwekesha ijumaa au jumamosi kwa funga

Swali: Ni ipi hukumu ya kufunga siku ya ijumaa?

Jibu: Kuipwekesha kwa funga haijuzu. Lakini akifunga pamoja nayo alkhamisi au jumamosi ni jambo linalofaa. Ingawa udhahiri wa dalili unaonyesha kuwa haijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Msiikhusishe siku ya ijumaa kwa funga baina ya masiku mengine na wala usiku wake kwa kusimama usiku baina ya nyusiku zengine.”

Kwa hivyo mtu akifunga pamoja nayo siku nyengine – ima siku moja kabla au baada yake – basi yanaondoka makatazo. Dalili juu ya hayo ni yale yaliyothibiti kwa Juwayriyyah kwamba alifunga siku ya ijumaa. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia:

”Jana ulifunga?” Akajibu: ”Hapana.” Akamuuliza tena: ”Umepanga kufunga kesho?” Akajibu: ”Hapana.” Ndipo akasema: ”Basi fungua.”

Imefahamisha kwamba ni sawa na yanaondoka makatazo endapo akifunga siku ya ijumaa na siku nyingine kabla au baada yake. Ndani yake pia kuna dalili juu ya kwamba ni sawa kufunga siku ya jumaosi. Kwa sababu alisema:

”Umepanga kufunga kesho?”

Kumepokelewa Hadiyth juu ya kufunga siku ya jumamosi. Amesema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Msifunge siku ya jumamosi japo ni kwa kutafuna gome la mti, basi alitafune.”

Lakini hata hivyo Hadiyth ni dhaifu. Baadhi ya wanachuoni wamesema kuwa ni Hadiyth ambayo baadhi wameipokea kwa njia inayotofautiana na ya wengine (Muttwarib). Wengine wakasema wameifasiri kwamba makatazo ni pale ambapo itapwekeshwa siku ya jumamosi. Lakini endapo mtu ataifunga na siku nyingine basi makatazo yatakuwa ni yenye kuondoka. Makatazo yamekuja kufunga siku ya jumamosi na kuipwekwesha.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (17)
  • Imechapishwa: 08/02/2021