Kuingiza TV na dishi/king´amuzi nyumbani ili watoto wasende kwa jirani

Swali: Kuna mwanamke aliye na watoto wawili ambao huenda kwa marafiki zao kutazama dishi na hukaa huko mpaka saa tisa usiku. Mwanamke huyu anaogopa kukaa nyumbani peke yake. Je, inajuzu kwake kuwanunulia dishi ili waweze kukaa nyumbani? Kwa sababu wanamwambia akiwanunulia nayo watabaki nyumbani. Anachelea juu yao wasije kupotea na kufikwa na yakuwafika.

Jibu: Ninaapa kwa Allaah kwamba mimi sina jibu juu ya hili. Kwa sabab dishi ni moto wenye mwako mkali. Je, hivyo itafaa kwangu kumjibu kwamba alete dishi ili ajiweke katika mtihani yeye mwenyewe na watoto wake? Hili ni gumu kwangu. Kule kwenda kwao kwa wengine ambao nyumbani kwao wana dishi wanasihi na wabainishie ukhatari wake juu ya dini yao na juu ya fikira zao. Lakini mimi siwezi kufutu kwamba wamiliki dishi. Kwa sababu lau yatakuwa ni kweli nusu tu ya yale ninayosikia kuhusu dishi hiyo, basi itatosha kukata moja kwa moja uharamu wa kuimiliki. Mwombe Allaah mwishoni mwa usiku ya kwamba Allaah awatengeneze watoto wako. Kwani Allaah (Jalla wa ´Alaa) yukaribu na Mwenye kujibu. Wanasihi. Hakuna neno ukawaletea TV. Lakini washurutishie wasiweke isipokuwa tu yale mambo yenye manufaa kama kwa mfano kutazama Makkah na al-Madiynah wanaposwali, taarifa ya khabari na ulimwengu katika kila mahali. Tunamuomnba Allaah amsaidie juu ya kuwalea.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (51) http://binothaimeen.net/content/1166
  • Imechapishwa: 03/07/2019