Kuingiwa na wasiwasi wa kukata au kuendelea na swalah baada ya kubishwa hodi au simu kuita


Swali: Mswaliji akisikia mtu anabisha hodi ambapo akasita kama akate swalah au asikate – swalah yake inabatilika?

Jibu: Kuna wanachuoni walioonelea kuwa swalah yake inabatilika hata kama hakuwa na azma ya kukata. Wanachuoni wengine wanaonelea kuwa swalah haibatiliki kwa kuingiwa na mashaka. Wanaonelea kuwa msingi ni kwamba nia bako ipo na kuingiwa na mashaka hakuibatilishi. Maoni haya ya pili ndio sahihi. Midhali hakuazimia kuikata basi bado yuko katika swalah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/450)
  • Imechapishwa: 05/08/2017