Kuingia na vitabu vya dini chooni


Swali: Inajuzu kwangu kuingia chooni na bafuni nikiwa na vitabu vidogo mfukoni?

Jibu: Imechukizwa kuingia na kitu chochote kilicho na utajo wa Allaah. Isipokuwa ikiwa kama anachelea wezi au vikapotea. Katika hali hiyo ndio anaweza kuingia navyo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (85) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17635
  • Imechapishwa: 28/06/2018