Kuingia chooni na makaratasi yaliyoandikwa jina la Allaah

Swali: Ni ipi hukumu ya kuingia chooni na makaratasi yaliyoandikwa jina la Allaah?

Jibu: Inajuzu kuingia chooni na makaratasi yaliyoandikwa “Allaah” maadamu yako mfukoni na hayaonekani. Yanatakiwa yawe yamefichika na kusitirika. Mara nyingi ni vigumu majina kusalimika na utajo wa Allaah. Kama vile ´Abdullaah, ´Abdul-´Aziyz na mfano wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/109)
  • Imechapishwa: 13/06/2017