Kuilazimisha nafsi kufunga wakati wa kupitwa na swalah

Swali: Kuna mtu amepitwa na swalah ya Fajr pamoja na mkusanyiko ambapo nikaiadhibu nafsi yake kufunga siku hiyo. Ni ipi hukumu ya kufanya hivo?

Jibu: Haitakiwi kusema kwamba umeiadhibu nafsi yako. Unachotakiwa kusema ni kwamba umeweka nadhiri. Ukiweka nadhiri ni jambo linafaa. Mwenye kupitwa na swalah ya Fajr, ikiwa hakukusudia kufanya hivo, basi hapati dhambi. Mtume mwenyewe (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walipitwa na swalah ya Fajr kama ilivyokuja katika Hadiyth siku ambayo walipigwa na jua. Kwa hiyo inafaa kwake kufanya hivo. Akifunga pasi na kuweka nadhiri ni katika matendo yaliyopendekezwa. Ama akiilazimisha nafsi yake nadhiri basi asisemi kuwa ameiadhibu nafsi yake. Bali aseme kuwa amefunga kwa ajili ya Allaah hali ya kumshukuru au kwamba amefanya matendo yanayofuta maovu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (08) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191309#219638
  • Imechapishwa: 09/02/2019