Kuichoma Qur-aan kwa kusahau na kwa kukusudia

Swali: Ni yepi malipo kwa mwenye kuchoma moto Qur-aan tukufu kwa kusahau na wala hakujua kitendo hicho isipokuwa baada ya kukifanya?

Jibu: Hakuna kinachomlazimu muda wa kuwa ameichoma kwa kusahau au ameichoma kwa kukusudia kwa sababu imechanikachanika na hanufaiki kwayo na hivyo akaichoma kwa sababu isitwezwe. Katika hali hiyo hakuna neno. Kwa sababu Qur-aan imekatikakatika na imechanikachanika na hanufaiki kwayo, inatiwa moto. Pia mtu anaweza kuifukia kwenye ardhi safi ili isitwezwe. Ikiwa aliichoma kwa kusahau hakujua kuwa ni Qur-aan hakuna dhambi kwake.

Ama akiichoma moto kwa sababu ya kuitukana au kwa sababu ya kuichukia anaritadi kutoka nje ya Uislamu. Kama anaichoma kwa sababu ya kuichukia na kuibughudhi ni dhambi kubwa na ni kuritadi kutoka nje ya Uislamu. Vivyo hivyo endapo ataikalia, akaikanyaga kwa miguu kwa ajili ya kuidharau au akaitupa katika najisi, matendo yote haya ni kuritadi kutoka nje ya Uislamu.

Akipatikana muislamu ambaye anaidharau Qur-aan waziwazi kama kwa mfano kwa kuikanyaga kwa miguu yake, akaikalia kwa makalio yake, akaitupa katika najisi au akaitukana, akamtukana yule anayeizungumza au mfano wa hayo ni kuritadi kutoka nje ya Uislamu. Ni kufuru kubwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: binbaz.org.sa/fatwas/7700/حكم-احراق-القران-سهوا-وعمدا
  • Imechapishwa: 02/05/2020