Kuhusu kitabu cha mbwa mwenye kubweka

Niliombwa mara nyingi kumraddi al-Qardhwaawiy. Mpaka hatimaye nikasikia anazungumza mambo ambayo hayatakiwi kunyamaziwa. Radd nimeipa jina katika mlolongo wa kwanza:

”Iskaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy” [Kumnyamazisha mbwa mwenye kubweka Yuusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy]

Ninamnasihi kila ndugu yule ambaye yuko na maneno au gazeti lolote kuhusu al-Qardhwaawiy atutumie – Allaah amjaze kheri.

Baadhi ya Hizbiyyuun watasema:

”Unamwita mwanachuoni miongoni mwa wanachuoni kuwa ni mbwa anayebweka. Hii si ni dhambi kubwa, ee Abu ´Abdir-Rahmaan? Mwanachuoni! Muftiy wa Qatar!”

Sikiliza Allaah (´Azza wa Jall) anavyosema:

وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ الَّذِي آتَيْنَاهُ آيَاتِنَا فَانسَلَخَ مِنْهَا فَأَتْبَعَهُ الشَّيْطَانُ فَكَانَ مِنَ الْغَاوِينَ وَلَوْ شِئْنَا لَرَفَعْنَاهُ بِهَا وَلَـٰكِنَّهُ أَخْلَدَ إِلَى الْأَرْضِ وَاتَّبَعَ هَوَاهُ ۚ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ الْكَلْبِ إِن تَحْمِلْ عَلَيْهِ يَلْهَثْ أَوْ تَتْرُكْهُ يَلْهَث ۚ ذَّٰلِكَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۚفَاقْصُصِ الْقَصَصَ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ

“Wasomee habari za yule Tuliyempa Aayah Zetu akajivua nazo. Shaytwaan akamfuata na [hatimaye] akawa miongoni mwa waliopotoka. Lau Tungelitaka tungelimnyanyua [kutoka utwevuni] kwazo [hizo Aayah], lakini aligandamana na dunia na akafuata matamanio yake. Basi mfano wake ni kama mfano wa mbwa, ukimhujumu ananing’iniza ulimi nje na kuhema, na ukimwacha kwa amani pia ananing’iniza ulimi nje na kuhema. Huo ndio mfano wa watu waliokadhibisha Aayah Zetu. Basi simulia visa huenda wakatafakari.” 07:175-176

مَثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا ۚ بِئْسَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ

“Mfano wa wale waliobebeshwa Tawraat halafu wasiibebe [kwa kuitendea kazi], ni kama mfano wa punda abebaye vitabu vitakatifu. Ubaya ulioje mfano wa watu waliokadhibisha Aayah za Allaah; na Allaah hawaongoi watu madhalimu.” 62:05

إِنَّ شَرَّ الدَّوَابِّ عِندَ اللَّـهِ الصُّمُّ الْبُكْمُ الَّذِينَ لَا يَعْقِلُونَ وَلَوْ عَلِمَ اللَّـهُ فِيهِمْ خَيْرًا لَّأَسْمَعَهُمْ ۖ وَلَوْ أَسْمَعَهُمْ لَتَوَلَّوا وَّهُم مُّعْرِضُونَ

“Hakika viumbe viovu kabisa mbele ya Allaah ni [hawa] viziwi na mabubu ambao hawatumii akili; na kama Allaah angelijua kuwa wana kheri yoyote, basi angeliwawezesha kusikia; na kama angeliwawezesha kusikia, wangeligeuka nao huku wakipuuza.” 08:22-23

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waad´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iskaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy, uk. 5-6
  • Imechapishwa: 08/10/2016