Kuhudhuria sherehe za harusi mahali kuna maovu ambayo mtu hatoyashiriki

Swali: Sherehe zetu nyingi huwa hazina mambo ya maovu isipokuwa tu wakati wanaume wanaingia kwenye ukumbi wa chakula ulio karibu na ukumbi wa wanawake ndipo wanaweza kusikia sauti za wanawake kwa jina “vigelegele”. Je, kitendo hichi ni maovu? Katika hali hii ni wajibu kwetu kutoka nje baada ya kuhudhuria katika chakula ilihali nafsi ni zenye kutamani chakula hichi na wanawake wamekataa kuzishusha sauti zao? Nikijua kuwa wanawake watafanya maovu katika harusi hii nisihudhurie na khaswa kwa kuzingatia kwamba mimi sintoshuhudia?

Jibu: Wanachuoni (Rahimahumu Allaah) wamesema kwamba mtu akiitwa katika karama ya ndoa na ndani yake kukawepo maovu asiyoweza kuyaondosha na wakati huohuo hatoyahudhuria, kuyashuhudia wala hatoyasikia, basi yuko na khiyari; akitaka atahudhuria na akitaka asihudhurie.

Kuhusu kwamba ukumbi wa wanawake uko karibu na ukumbi wa wanaume, nashauri kwamba ukuta unaotenganisha kati ya ukumbi wa wanaume na wanawake uwe umefungwa na sauti isize kutoka nje. Vilevile sauti ikhafifishwe cha kiwango cha wale wanawake walioko ukumbini tu kuweza kusikia. Watu wakiyafanyia kazi haya kwa njia ya kwamba wanawake wakawa kivyao na hali ya kufungwa ambapo sauti haiwafikii wanaume na pia sauti ikawa ndani ya ukumbi pekee, hakuna neno. Katika hali hii ahudhurie na hakuna neno juu yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (66) http://binothaimeen.net/content/1472
  • Imechapishwa: 18/01/2020