Kuhudhuria mahali kunapofanywa uchawi na mazingaombwe

Swali: Kuna muulizaji kutoka nje katika nchi ya kikafiri ambaye anasema kuwa wanaonyesha hadharani michezo ya kichawi na mazingaombwe. Ni ipi hukumu ya kutazama hayo?

Jibu: Haya yapo hata Malaysia, India na sehemu nyingi.

Swali: Vipi hukumu ya kuhudhuria na kutazama?

Jibu: Haijuzu. Isipokuwa kwa yule anayetaka kuyakemea na kubainisha hukumu yake.

Swali: Inajuzu kwenda kwa ajili ya kutaka kujiliwaza kidogo?

Jibu: Hapana, haijuzu. Ni dhambi. Isipokuwa kwa yule anayetaka kuyakemea ili watu watahadhari nayo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://ia802700.us.archive.org/3/items/Ketab_Taw7eed_Ibn_Baz/27.mp3
  • Imechapishwa: 07/10/2018