Kuhisi uzito wakati wa kusoma Tawhiyd


Swali: Watu wengi wanasikiliza kaseti kuhusu Siyrah na mengineyo, lakini nafsi zao zinahisi uzito wanaposikiliza kaseti kuhusu Tawhiyd.

Jibu: Allaah awaongoze. Allaah awaongoze waislamu waliopotea. Hakuna anayehisi uzito na Tawhiyd isipokuwa mnafiki au mtu mwenye Imani dhaifu.

Vilevile malezi yana umuhimu wake. Watoto wa waislamu wakilelewa juu ya kutoitilia umuhimu Tawhiyd wanakuwa ni wenye kuiona nzito. Lakini lau wangelilelewa na wakakuzwa juu yake, wangeliipenda na ingeliwakuwia rahisi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (61) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13585
  • Imechapishwa: 16/11/2014