Swali: Ni ipi hukumu muislamu akiharibu nguzo moja miongoni mwa nguzo za imani sita?

Jibu: Akiharibu nguzo moja miongoni mwa nguzo za imani sita hali ya kuwa ni mjinga na mwenye kukadhibisha ni kafiri. Ama ikiwa ni kwa kupindisha maana, kama wale waliopinga mambo kadhaa katika mlango wa Qadar, huyu hakufuru. Kwa sababu ni mwenye kupindisha maana. Lakini wakati fulani kupindisha maana kunakuwa mbali na wakati mwingine kunakuwa karibu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (377) http://binothaimeen.net/content/13369
  • Imechapishwa: 26/09/2020