Kuharibika kwa waislamu hii leo – alama ya Qiyaamah?


Swali: Kuharibika hali za waislamu ni miongoni mwa alama za Qiyaamah?

Jibu: Hakusemwi kitu juu ya alama za Qiyaamah isipokuwa yale yaliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam); ima yawe yamekuja katika Qur-aan au yawe yametoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakusemwi hili kuwa ni katika alama za Qiyaamah ilihali halina dalili yoyote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14005
  • Imechapishwa: 18/04/2018