Kuhakikisha kwanza kabla ya kumkufurisha muislamu


Swali: Yule mwenye kutenda moja katika vitenguzi vya Uislamu anakufurishwa na kila mwenye kumuona au hakuna anayemkufurisha isipokuwa wanachuoni tu?

Jibu: Yule mwenye kutenda moja katika vitenguzi vya Uislamu inatakiwa kwanza kuhakikisha juu ya jambo lake. Huenda akawa mjinga anayepewa udhuru kwa ujinga. Huenda akawa ametenzwa nguvu. Huenda akawa na udhuru. Ikishahakikishwa kwamba hana udhuru wowote na kwamba sio mjinga basi atahukumiwa kwa vile inavyopelekea haki yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 33
  • Imechapishwa: 11/05/2018