Kugeuza nia ya swalah ya sunnah kwenda swalah ya faradhi

Swali: Akiingia mtu msikitini baada ya kumalizika swalah ya mkusanyiko na hivyo akataka kuswali swalah ya sunnah, akasema “Allaahu Akbar” na kabla ya kusoma al-Faatihah akaingia mtu mwingine na kupanga naye safu na kumfanya kuwa imamu. Je, inafaa kwake kugeuza nia yake kutoka katika swalah iliyopendekezwa na kwenda katika swalah ya faradhi? Swalah yake itasihi?

Jibu: Haifai kwake kufanya hivo. Anachotakiwa kufanya ni kukamilisha swalah yake y sunnah kisha baada ya hapo ndio aswali faradhi. Swalah ya faradhi ni lazima kwa mtu aanze kuinuia kuanzia mwanzo wake na si kugeuza nia katikati ya swalah kutoka katika swalah iliyopendekezwa na kwenda katika faradhi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (19)
  • Imechapishwa: 13/03/2021