Swali: Nimewasikia wanaosema kwamba imechukizwa kufuta mchanga kwenye paji la uso baada ya kumaliza kuswali. Je, kitendo hichi kina msingi?

Jibu: Hakina msingi kutokana na tunavotambua. Imechukizwa kufanya hivo kabla ya salamu. Kwa sababu imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika baadhi ya swalah zake kwamba alitoa Tasliym kutoka katika swalah ya Fajr katika usiku wa mvua na kukaonekana usoni mwake athari za maji na udongo. Hiyo ni dalili inayojulisha kutokupangusa kabla ya kumaliza swalah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/198)
  • Imechapishwa: 30/10/2021