Kufuta jina la Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab katika vitabu vyake


Swali: Sauti ina chenga sana na tumechoweza kusikia ni wanafunzi waliosoma Saudi Arabia wanauliza kama inafaa kufuta jina la Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab kutoka kwenye vitabu vyake kama ”al-Usuwl ath-Thalaathah” na vyenginevyo pindi wanaporudi katika miji yao kwa sababu watu wanamchukia…

Jibu: Haijuzu kufuta jina la Shaykh. Huu ni mwenendo mbaya. Kufuta jina la mtunzi na kuliondosha katika vitabu ni jambo lisilojuzu. Bali linatakiwa kubaki. Yule atakayekubali, kheri ni kwake, na yule asiyekubali, uongofu uko mikononi mwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kinachowapotosha sio jina la Shaykh. Kinachowapotosha ni shaytwaan na kufuata matamanio. Mwenendo huu wa kufuta jina kamilifu la Shaykh na badala yake kuandika ”Muhammad at-Tamiymiy” ni kosa kubwa. Mwandishi asifutwe kutoka kwenye kitabu chake. Vinginevyo hili litapelekea kuviharibu vitabu vyengine pia pamoja na vitabu vya Salaf, kufutwa majina yao, kufutwa baadhi ya maneno yao ambayo yule mfutaji anaona kuwa yanawakimbiza watu. Tusifanye hivo. Hii ni khiyana ya kielimu. Jina la Shaykh linatakiwa kubaki katika kitabu chake. Yule mwenye kukubali haki, himdi zote anastahiki Allaah, yule asiyekubaki, hoja imemsimamia. Shaykh hakuja na maneno kutoka kwake mwenyewe. Katika vitabu vyake anasema yaliyotajwa, Allaah na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanachuoni. Hakuja na maneno kutoka kwake mwenyewe na kupingana na wanachuoni wa waislamu. Bali anafuata njia ya wanachuoni wa as-Salaf as-Swaalih.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Masaa´il-il-Jaahiliyyah (01) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/jahlyh_01.mp3
  • Imechapishwa: 18/11/2017