Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema kwamba ukafiri ni kule kukadhibisha?

Jibu: Huu ni ujinga. Ni ujinga uliopandiana. Lau atamtukana Allaah au akamkadhibisha hakufuru?

Swali: Je, si anatoka nje ya Uislamu?

Jibu: Ndio, anakuwa kafiri. Wale ambao wanaona kuwa kufuru ni kukadhibisha pekee maana yake ni kwamba anayeswali kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, akamsujudia asiyekuwa Allaah au akamtukana Allaah hakufuru midhali hakadhibishi .

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 58
  • Imechapishwa: 29/06/2019