Swali: Je, Niqaab kwa mwanamke ni lazima au imependekezwa tu? Je, Niqaab ni maalum kwa mama wa waumini peke yao au ni kwa wanawake wote? Je, inafaa kwa mwanamke  kuonyesha uso na viganja vya mikono?

Jibu: Niqaab ni yenye kuwahusu watu wote kuanzia mama wa waumini na wanawake wengine. Mwanzoni mwa Uislamu Hijaab ilikuwa sio lazima. Kisha hilo likafutwa na Allaah akateremsha maneno Yake (Ta´ala):

وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ ذَٰلِكُمْ أَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَقُلُوبِهِنَّ

“Mnapowauliza haja, basi waulizeni nyuma ya pazia. Hivyo ni utwaharifu zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao.” (33:59)

وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ

“Na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, baba zao, baba za waume wao, wana wao wa kiume… “ (24:31)

Ndipo Hijaab ikalazimika kwa watu wote. Ni mamoja kwa Niqaab au kitu kingine. Ni mamoja Niqaab ambayo inawekwa usoni na kunaachwa upenyo kwa ajili ya jicho moja au penyo mbili kwa ajili ya macho mawili peke yake au kwa kujiteremshia mtandio juu ya uso mzima.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb https://binbaz.org.sa/fatwas/9564/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%86%D9%82%D8%A7%D8%A8-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A7%D8%A9
  • Imechapishwa: 20/04/2020