Kufungua maji kitambo kifupi ili yaje maji ya moto

Swali: Wakati wa majira ya baridi wakati fulani kabla ya kutawadha au kuoga tunaacha maji yabubuje kidogo ili yaje maji yenye moto. Je, tunapata dhambi? Je, inazingatiwa ni israfu?

Jibu: Hapana. Hili ni kutokana na udhuru. Unafungua ili yaondoke maji ya baridi na yaje maji ya moto hakuna neno kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (107) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighatoulahfan-22-06-1441.mp3
  • Imechapishwa: 31/08/2020