Kufungua maduka kabla ya watu hawajamaliza kuswali ijumaa

Swali: Kuna baadhi ya wamiliki wa maduka ambao wanaenda siku ya ijumaa katika misikiti inayofungua mapema. Halafu baada ya hapo wanafungua maduka yao karibu na misikiti mingine ambayo haijaswali ijumaa. Kwa njia hiyo duka hilo lililo karibu na msikiti linakuwa limefunguliwa. Ni ipi hukumu ya kufanya hivo? Je, wakemewe?

Jibu: Hili linarudi kwa wale walinzi wa usalama inapokuja katika kuwakataza au kutowakataza. Kuhusu upande wa kutekeleza swalah ya ijumaa wamekwishaiswali na wala hawataombwa kuiswali tena. Lakini sio katika mambo yaliyopendekezwa kabisa kufungua maduka yao sokoni ambapo kunaswaliwa swalah ya ijumaa. Kwa kuwa katika hili kuna kitu katika kuvuka mpaka na mtu kutojali. Jengine ndani ya kitendo hichi kuna kujijengea wao wenyewe dhana mbaya.

Naona kuwa wanatakiwa kuswali katika msikiti ambao uko karibu na wao mpaka pale watu watapomaliza watasimama na kutoka, kama alivyosema (Ta´ala):

فَإِذَا قُضِيَتِ الصَّلَاةُ فَانتَشِرُوا فِي الْأَرْضِ وَابْتَغُوا مِن فَضْلِ اللَّـهِ

“Inapomalizika swalah, basi tawanyikeni katika ardhi na tafuteni katika fadhilah za Allaah.”[1]

Kuhusu kitendo cha wao kufungua maduka ilihali watu walioko misikitini ilioko pembezoni mwao bado wanaswali ni jambo linarudi kwa wale walinzi wa usalama.

[1] 62:10

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthyamiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (40) http://binothaimeen.net/content/905
  • Imechapishwa: 14/06/2019